Mgeni wetu ni Ghislain PALUKU BAMBIRIKIRE, katibu mkuu wa Chama cha Walimu wa Kongo (SYECO) katika jiji la Beni. Kufuatana na wito wa SYECO ya kitaifa, madarasa yalianza tena hii siku ya kwanza tarehe makumi mbili na moja Oktoba katika shule za umma za jiji hilo, lakini kwa idadi iliyopunguzwa. Je, tunapaswa kufanya tathmini gani kuhusu kurejeshwa huku kwa shule tangu kuanza kwa mgomo tarehe mbili Septemba? Ghislain PALUKU BAMBIRIKIRE, katibu mkuu wa Syeco katika mji wa Beni, anatueleza kuhusu hilo katika mahojiano haya na André KITENGE.
Source: Radio Okapi